top of page

Safari ya Uhai

Public·45 members


Haijalishi mkeo anafanya kazi na anapata pesa au hafanyi kazi, jukumu la kumtunza yeye na familia yako ni lako wewe mwanaume. Hii haimaanishi mwanamke hana mchango, bali ina onyesha nafasi yako kama kiongozi wa familia kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana na nyumba inasimama imara. Mwanaume halisi hapimi majukumu kwa kipato cha mke wake, anasimama kwenye wajibu wake bila kisingizio. Mke akichangia, iwe ni baraka ya kusaidia maendeleo, sio sababu ya wewe kupunguza wajibu wako, msingi mzuri wa nyumba unaanzia kwako mwanaume. Jifunze kuwajibika, kupanga na kusimamia familia yako kwa busara. Heshima ya mwanaume ina onekana kwenye namna anavyo linda na kutunza familia yake.


Kumbuka: Uwajibikaji wako ndio msingi wa utulivu wa familia simama imara hata kama hali ni ngumu.

2 Views
bottom of page