MBU DUME

Google wanapanga kuachia mbu milioni 32 kwenye miji ya Florida na California
Subiri kwanza hii sio movie
Kabla hujasema ni njama za mabeberu hebu elewa kwanza mchezo ulivyo
Hawa sio mbu wa kawaida unaowajua wewe
IPO HIVI


Google wanapanga kuachia mbu milioni 32 kwenye miji ya Florida na California
Subiri kwanza hii sio movie
Kabla hujasema ni njama za mabeberu hebu elewa kwanza mchezo ulivyo
Hawa sio mbu wa kawaida unaowajua wewe
IPO HIVI

Kuna muda huwa unafika, automatic unajikuta huna tena zile shobo na mapenzi ya kupitiliza.😔💔
Kichwa kinawaka moto kuwaza maisha yako na mwelekeo wako. Unaanza kuona vitu kwa uhalisia zaidi kuliko hisia. Simu hata isipoingia meseji ya mtu kukusalimia unaona fresh tu, hauumii tena kama zamani. Ndugu wakikutenga unaona sawa tu, kwa sababu unaanza kuelewa kuwa sio kila mtu ana nafasi ya kudumu kwenye maisha yako.
Unashangaa unapunguza kujali mambo yasiyo kuhusu, unaanza kuchagua amani yako kuliko drama za dunia. Moyo unakuwa mgumu kidogo, lakini akili inakuwa imetulia zaidi. Hii ni hatua ya kukua kiakili na kihisia. Unaanza kujitambua, kujipa thamani na kuelewa kuwa sio kila kitu kinahitaji nguvu zako. Unachagua kupambana na maisha yako, ndoto zako na future yako, badala ya kupoteza muda kwa mambo yasiyo na maana.
Kumbuka: Sio kwamba umekuwa mbaya au hauna mapenzi tena, bali umefikia hatua ya kujilinda na kuchagua kile chenye maana kwenye maisha yako.…

Unakuwa na mwanaume ambaye, hata ukimueleza shida zako hakusaidii… sasa huyo ni mume au sanduku la maoni? 😂💔
Maana ndoa au mahusiano siyo sehemu ya kusikilizana tu bila hatua, bali ni sehemu ya kusaidiana na kusimama pamoja kwenye changamoto. Inaumiza pale unapo fungua moyo wako ukitegemea msaada au ushirikiano, lakini mwenzako anabaki kimya au anakupa majibu ya juu juu bila kujali uzito wa tatizo.
Mwanaume wa kweli hatakiwi kuwa msikilizaji tu, bali pia awe mshirika wa maisha—mtu wa kukupa faraja, ushauri na msaada pale inapo wezekana. Sio lazima awe na kila suluhisho, lakini angalau aonyeshe kujali na kuchukua hatua hata kidogo.
Kama kila kitu unakibeba peke yako huku yeye yupo kama mtazamaji, ni muhimu kujiuliza nafasi yake kwenye maisha yako ni ipi. Mahusiano yana hitaji ushirikiano, sio mtu mmoja kupambana na mwingine kutazama. Mwisho wa siku, mume au mwenza anatakiwa kuwa nguzo ya nguvu na faraja, sio mtu wa kukusikiliza…

Unaweza kumchafua mtu kwa kumtangazia mabaya kila sehemu, lakini huwezi kuzuia riziki zake alizo pangiwa na MUNGU.❤️
Watu wanaweza kusema, kupanga na hata kujaribu kukushusha, lakini kile ambacho Mungu ame kikusudia kwako hakizuiliki na maneno wala hila za binadamu. Usipoteze muda kujitetea kwa kila mtu, endelea na njia yako, fanya kazi zako kwa bidii na uache matokeo yaongee. Ukweli una tabia ya kujitokeza hata ukifichwa kwa muda.
Wanao kuchafua wanaweza kukufanya uonekane vibaya kwa watu, lakini hawawezi kubadilisha hatima yako. Riziki yako iko mikononi mwa Mungu, sio midomoni mwa watu.
Kumbuka: Heshima yako inaweza kujaribiwa na maneno ya watu, lakini mafanikio yako yana lindwa na mipango ya Mungu. Endelea kusonga mbele bila kuangalia nyuma.
Nikutakie Usiku Mwema mwanasafari ya uhai.🥰