Unakuwa na mwanaume ambaye, hata ukimueleza shida zako hakusaidii… sasa huyo ni mume au sanduku la maoni? 😂💔
Maana ndoa au mahusiano siyo sehemu ya kusikilizana tu bila hatua, bali ni sehemu ya kusaidiana na kusimama pamoja kwenye changamoto. Inaumiza pale unapo fungua moyo wako ukitegemea msaada au ushirikiano, lakini mwenzako anabaki kimya au anakupa majibu ya juu juu bila kujali uzito wa tatizo.
Mwanaume wa kweli hatakiwi kuwa msikilizaji tu, bali pia awe mshirika wa maisha—mtu wa kukupa faraja, ushauri na msaada pale inapo wezekana. Sio lazima awe na kila suluhisho, lakini angalau aonyeshe kujali na kuchukua hatua hata kidogo.
Kama kila kitu unakibeba peke yako huku yeye yupo kama mtazamaji, ni muhimu kujiuliza nafasi yake kwenye maisha yako ni ipi. Mahusiano yana hitaji ushirikiano, sio mtu mmoja kupambana na mwingine kutazama. Mwisho wa siku, mume au mwenza anatakiwa kuwa nguzo ya nguvu na faraja, sio mtu wa kukusikiliza…