Kwahiyo unaniambia tulifanya vyote vile, ili tusije kuongea tena milele?😭💔

Zile simu za usiku mkubwa, tulizo tegeana ni nani wa kuzikata...
Zile ahadi za utanifanya niwe mume mwenye bahati zaidi mbele yako...
Ile mitoko ya usiku, ya kujirekodi kila tukio ukicheka huku unanieleza namna unavyo nipenda.
Zile video call ukiwa mbali na maneno ya unatamani ningekuwa karibu yako..
Vyote tulifanya ili leo tusijuliane hali na kila mtu afute namba ya mwenzie? Nakuuliza..
Lile kumbato la usijali muda ambao dunia imenielemea..
Zile meseji za usiku mwema, zilizo endelea kuwa chat ndefu mpaka kufikia kulala bila kuagana..
Nieleze, tulifanya vyote ili tusiongeleshane tena leo hii? Kila mmoja awe mgeni wa mwenzie? Inaniumiza sana.
Anyway nikutakie usiku mwema.😔🙏
3 Views
