top of page

Safari ya Uhai

Public·45 members

Ukweli ambao wanapaswa kuufahamu dada zetu, sponsor hatoi maisha..💔


Hawezi kukupa uchumi utakaokupa uhuru wa kujitegemea, kwake hiyo ni sawa na yeye kujipiga risasi ya mguu..


Anajua unachompendea ni Pesa, kwa kuzingatia hili atahakikisha unapata Pesa ya kujikimu tu. Sio ya maendeleo kwaajili ya kesho yako.


Hapa ndipo huwa zinakuja kesi nyingi za ameninunulia iphone 16 ya zawadi. Lakini nikimwambia anifungulie biashara ananikwepa.


Atakupangia apartment kali, kodi laki 5, ambayo anajua ukiachana nae huwezi kulipa. Anaku-spoil kwenye hotel za gharama, lakini hela ya nauli anayokupa wewe kurudi kwako haifiki hata nusu ya chumba cha usiku mmoja..


Atakuchukua na kukupeleka vacation ku-enjoy bata kali, lakini hawezi kukujengea msingi imara wa wewe kujitegemea bila uwepo wake..


Ni very tricky, ukiwa kwenye raha huwezi kuyaona haya na mbaya zaidi najua huwezi kunielewa pia kwa sasa. Enjoy.

2 Views
bottom of page