KUMCHAFUA MTU

Unaweza kumchafua mtu kwa kumtangazia mabaya kila sehemu, lakini huwezi kuzuia riziki zake alizo pangiwa na MUNGU.❤️
Watu wanaweza kusema, kupanga na hata kujaribu kukushusha, lakini kile ambacho Mungu ame kikusudia kwako hakizuiliki na maneno wala hila za binadamu. Usipoteze muda kujitetea kwa kila mtu, endelea na njia yako, fanya kazi zako kwa bidii na uache matokeo yaongee. Ukweli una tabia ya kujitokeza hata ukifichwa kwa muda.
Wanao kuchafua wanaweza kukufanya uonekane vibaya kwa watu, lakini hawawezi kubadilisha hatima yako. Riziki yako iko mikononi mwa Mungu, sio midomoni mwa watu.
Kumbuka: Heshima yako inaweza kujaribiwa na maneno ya watu, lakini mafanikio yako yana lindwa na mipango ya Mungu. Endelea kusonga mbele bila kuangalia nyuma.
Nikutakie Usiku Mwema mwanasafari ya uhai.🥰
