top of page

Safari ya Uhai

Public·45 members

WEWE UNAWEZA

‎Kuna siku unaamka asubuhi una nguvu za kufanya mambo makubwa, unajiona kama simba wa porini. ‎Lakini baada ya dakika 10 tu unaangalia simu unaona watu wana onyesha mafanikio yao mtandaoni na ghafla unaanza kujiona kama mbuzi aliye potea sokoni sio simba tena. ‎Hadi unaanza kusema "Mimi siwezi..." ‎Lakini swali ni kweli huwezi au umejikatia tamaa mapema? ‎Maisha ya sasa yanatufanya tuamini kwamba mafanikio ni kitu cha haraka, unaona mtu ameanza biashara leo, kesho ana onekana kwenye gari la kifahari. ‎Unaona mtu amefungua account YouTube mwezi mmoja haraka tu ana subscribers wengi unatamani kuwa kama yeye unasahau kuna zile siku alikua anapost video halafu wanaotazama ni yeye mwenyewe familia na jirani mmoja.

‎Ukweli ni kwamba kila mtu mkubwa alianza akiwa mdogo, hakuna mtoto aliye zaliwa anajua kuendesha baiskeli. ‎Mara ya kwanza wengi huanguka hadi kutoa vidonda lakini hawakuacha kujifunza kila siku, hata kwenye maisha halisi ipo hivyo. ‎Mwanafunzi aliyepata alama nzuri hakuanza akiwa anafahamu kila kitu, hata mfanyabiashara aliye fanikiwa hakuanza akiwa na mamilioni. ‎Kuna watu wengi wana shindwa si kwa sababu hawawezi wana shindwa kwa sababu wamejihakikishia mapema kwamba hawawezi. ‎Amini kwamba Wewe unaweza....

Unaweza kuanza biashara ndogo, kujifunza kitu kipya, kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na pia unaweza kushinda hofu zako. ‎Usisubiri mpaka siku ambayo utaona una nguvu asilimia 100 kwa sababu siku hiyo haiwezi kufika, anza na asilimia 20 uliyonayo leo.

  • Kumbuka: Safari ndefu haianzi kwa mipango bila vitendo inaanza kwa hatua, ‎kwa hiyo jiulize kama wengine waliweza, kwa nini wewe usiweze?

5 Views
bottom of page