“Kuna watu wanakushika… lakini hawakupendi.”

Kuna kipindi nilikuwa naamini kwamba ukiona mtu anakutafuta sana, ana kutamani, anakugusa kwa hisia nyingi… basi huo ndio upendo. Nilikuwa naamini ukaribu wa mwili una maanisha ukaribu wa moyo. Lakini maisha yalinifunza kitu tofauti sana. Sio kila anaye kushika anakujali. Wengine wanataka tu kujaza upweke wao kupitia wewe. Wanataka kuhisi kuna mtu karibu nao usiku, lakini si kwa sababu wamekupenda kwa dhati. Na kibaya zaidi, unapo kuwa mtu mwenye moyo wa kweli, huwa ni rahisi sana kuchanganya attention na mapenzi.
Nakumbuka kuna siku nilikaa na mtu mmoja karibu sana, lakini ndani nilihisi upweke kuliko hata nilivyo kuwa peke yangu. Tulikuwa tunacheka, tuna gusana, tunaongea… lakini kuna sehemu ya moyo wangu ulikuwa una nong’ona kimya kimya, “Hapa kuna kitu kina kosekana.” Na unajua kitu gani huwa kinauma zaidi? Ni pale unapo gundua mtu alikuwa ana hitaji uwepo wako lakini si wewe.
Alikuwa anahitaji comfort.
Alikuwa anahitaji distraction.
Alikuwa anahitaji mtu wa kumfanya asijisikie mpweke.
Lakini hakuwahi kukaa chini kujiuliza moyo wako unahitaji nini. Sasa nikuulize… Umewahi kuwa karibu sana na mtu, lakini bado ukahisi kama hauonekani? Umewahi kuhisi unatoa hisia za kweli kwa mtu ambaye alikuwa anacheza tu na emptiness yake? Kwa sababu watu wengi hawapo kwenye mahusiano kwa sababu ya upendo. Wapo kwa sababu hawawezi kuvumilia ukimya wa maisha yao wenyewe. Na hapo ndipo watu wana umizana.
Mtu ana kushikilia kwa nguvu, ana kufanya ujisikie wa muhimu, anakupa attention ya kila siku halafu siku anapo pata amani yake au distraction nyingine, ghafla unakuwa kama hukuwahi kuwepo. Na wewe unabaki ukijilaumu, ukijiuliza kosa lako lilikuwa nini. Lakini ukweli ni kwamba, tatizo halikuwa wewe. Tatizo uliingia na moyo, wakati mwingine aliingia na hisia za muda. Na hiyo ndiyo picha hii ilinifanya nihisi. Mikono ile ina onekana ya karibu sana, lakini pia ina onekana nzito. Kama kuna mtu ana shikiliwa zaidi ya anavyo pendwa. Kama kuna kitu kina mvuta abakie, hata kama ndani yake amechoka.
Maisha yana tabia ya kutufundisha kwa njia ngumu sana kwamba si kila anayesema “nakuhitaji” ana maanisha “nakupenda.” Wengine wana hitaji uwepo wako tu ili wajisikie hai kidogo. Ndiyo maana siku hizi nimejifunza kuangalia zaidi matendo kuliko mguso. Kwa sababu mguso unaweza kudanganya. Maneno yanaweza kudanganya. Lakini namna mtu anavyo kutunza ukiwa dhaifu hapo ndipo ukweli huonekana. Na labda somo kubwa kabisa ni hili…
Usikubali kushikiliwa na mtu ambaye hana mpango wa kushika moyo wako kwa uaminifu. Kwa sababu mwisho wa siku, si kila ukaribu ni upendo na si kila anaye kukumbatia ana ogopa kukupoteza.
