KWA NINI KUMTAKIA MTU MABAYA HUZUIA BARAKA ZAKO

Ngoja niliongeze jambo lingine ambalo watu wengi hawalijui. Katika ulimwengu wa kiroho kuna kanuni ya ajabu sana: moyo wa mtu ndio mlango wa baraka zake.Sasa tatizo linatokea pale mtu anapoanza kubeba:
Chuki
Kisasi
Tamanio la kumwona mwingine akianguka.
Bila kujua, anakuwa amefunga mlango wa baraka zake mwenyewe.
1. Chuki Ni Mzigo wa Kiroho
Chuki ina tabia ya kumfunga kwanza anayeibeba. Ndiyo maana utaona mtu anasema anamchukia fulani, lakini ukweli ni kwamba:
Analala akimfikiria
Anaamka akimfikiria
Moyo wake hauna amani.
Hapo ndipo unapogundua kwamba chuki imeanza kumtawala yeye mwenyewe.
2. Baraka Hupenda Moyo Mwepesi
Katika mambo ya kiroho, baraka hupenda sana kukaa kwa mtu ambaye moyo wake:
Hauna visasi
Hauna chuki
Haupangi mabaya kwa wengine.
Hii ndiyo sababu watu wa zamani walikuwa wakisema:
“Usipigane na mtu moyoni, utaanza kupigana na baraka zako.” Kwa sababu baraka zinahitaji nafasi safi ya kukaa.
3. Haki ya Mungu Hufanya Kazi Bila Kusaidiwa
Watu wengi wanadhani lazima wafanye kitu ili mtu aliyewadhuru aone matokeo ya ubaya wake. Lakini ukweli ni huu: Haki ya Mungu haichelewi, na haihitaji kusaidiwa na kisasi cha binadamu. Mara nyingi mtu anayefanya ubaya:
Matokeo yake humfuata mwenyewe
Maisha humfundisha kwa njia yake.
Na wewe ukibaki na moyo safi, utaendelea mbele bila mzigo.
4. Siri ya Moyo Ulio Huru
Mtu anayejifunza kuachilia chuki hupata vitu vitatu muhimu:
Amani ya ndani
Ulinzi wa kiroho
Milango ya baraka kufunguka
Kwa sababu roho yake haibebi mzigo wa giza. Kabla hujamwombea mtu mabaya, kumbuka jambo hili:
1. Kila chuki unayoibeba ni kama jiwe unaloweka ndani ya mfuko wako mwenyewe.
2. Kadri unavyobeba mawe mengi, ndivyo safari yako ya maisha inavyokuwa nzito.
Ndiyo maana mimi Yusuf Mgunya mtu wa hekima nasema:
“Achilia chuki, ili baraka zipate nafasi ya kukufuata.”
